Tunatemblea Wagonjwa Kila Jumatano ya Kwanza wa Mwezi
Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa ni moja ya sakramenti za uponyaji katika Kanisa Katoliki, na nyingine ikiwa ni Sakramenti ya Kitubio. Sakramenti ya Mpako wa Wagonjwa ni alama ya nje ya neema ya Mungu inayolenga kuwapa wagonjwa nguvu ya kiroho na kimwili, ikiwa na msingi wake mkuu katika (Yak. 5:14-15). Katika aya hizi, Maandiko Matakatifu yanahimiza kwamba mgonjwa anapaswa kuwaita wazee wa Kanisa (Mapadre) ili wamwombee na kumpaka mafuta kwa jina la Bwana, kitendo ambacho huleta uponyaji wa nafsi na afya ya mwili, ambayo ni mapenzi ya Mungu. Sakramenti hii si “upako wa kifo” pekee, bali ni sala ya imani inayomuunganisha mteswa na mateso ya Kristo, ikimpa faraja ya Roho Mtakatifu dhidi ya vishawishi vya kukata tamaa au hofu ya mauti, na kumpatia ondoleo la dhambi kama hawezi kuungama.
Zaidi ya hayo, msingi wa huduma hii unaonekana katika utume wa Bwana wetu Yesu Kristo mwenyewe na agizo lake kwa mitume (Mk. 6:13), ambapo Maandiko yanasema “walitoa pepo wengi na wakapaka mafuta watu wengi waliokuwa wagonjwa wakawapoza.” Hii inaonyesha kuwa mpako huu ni mwendelezo wa huruma ya Kristo kwa binadamu anayetaabika, ukithibitisha kuwa Kanisa halimwachi mwana wake katika kipindi cha udhaifu mkubwa. Kumbe kupitia matumizi ya mafuta yaliyobarikiwa na Askofu (Mafuta ya Wagonjwa) katika adhimisho la Misa ya kubariki mafuta, Kanisa linaweka wazi kuwa neema ya Mungu inapenya hata katika maumivu, likimhakikishia mgonjwa kuwa yuko mikononi mwa Kristo aliyeshinda mauti, jambo linalompa mgonjwa utulivu wa ndani na tumaini la uzima wa milele.
Lorem ipsum dolor sit amet, consectetur adipiscing elit. Ut elit tellus, luctus nec ullamcorper mattis, pulvinar dapibus leo.
Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga Usa River ilianzishwa mnamo mwaka 1975 chini ya mapadre wa shirika la Roho Mtakatifu ikiwa na vigango 9 ikihudumia jamii ya Usa River na maeneo jirani.