Kuhusu Sisi

Historia ya Parokia

Kuanzishwa kwa Parokia

Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga Usa River ilianzishwa mnamo mwaka 1975 chini ya mapadre wa shirika la Roho Mtakatifu ikiwa na vigango 9 ikihudumia jamii ya Usa River na maeneo jirani. Vigango hivyo ni Mbuguni, Shambarai, Mererani, Valeska na Maji ya Chai. Kati ya vigango hivyo, vigango vine vimekuwa parokia. Vigango vilivyokuwa parokia ni Mbuguni, Kikatiti, Mererani, Ngurdoto na Maji ya Chai.

Mapadre Na Utume Katika Parokia Ya Mtakatifu Karoli Lwanga

Kwa sasa Parokia ya Mt. Karoli Lwanga inayohudumiwa na mapadre wa shirika la Roho Mtakatifu ina vigango 5 na kituo cha sala kimoja ambavyo ni:-

Kigangoa cha Mt. Joachim na Anna – Ngongongare
Kigango cha Mt. Augustino – Magadirish
Kigango cha Mt. Joseph Mfanyakazi – Nshupu
Kigango cha Mt. Stephano Shahidi – Kwaugoro
Kigango cha Mt. Patris – Momela
Kituo cha sala cha Moyo Safi wa Bikira Maria – Kiwawa

Jumuiya Ndogondogo

Parokia ya Mt. Karoli Lwanga Usa River ina jumuiya zipatazo 63.

Jiografia ya Parokia

Parokia ya Mt. Karoli Lwanga Usa River imepakana na Parokia ya Maji ya Chai kwa upande wa Mashariki, upande wa Magharibi imepakana na Parokia ya Poli Sing’isi, kwa upande wa Kaskazini imepakana na Parokia ya Ngurdoto sanjari na Mlima Meru na upande wa kusini imepakana na Parokia ya Nambala na Mbuguni.

Hali ya waumini na jamii ya Parokia

Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga in wakazi wa makabila mbalimbali, wengi wa wakazi ni kutoka katika mikoa yajirani ambao wanajishughulisha na kilimo, biashara, fugaji na ajira katika sekta mbalimbali. Lugha kuu ya mawasiliano ni Kiswahili japo kuna lugha nyingine zinazozungumzwa wka kiasi kidogo.

Hali ya wakazi wa Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga kiuchumi na kijamii ni wastani kwani imezungukwa na mashamba, biashara mbalimbali na huduma za kijamii.

Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga imejenga na kudumisha mahusiano mazuri na jamii nzima bila kujali ukabila, udini, jinsia na kuthamini huduma, michango itolewayo na wadau mbalimbali.

Dira ya Parokia ya Mtakatifu Karoli Lwanga

Familia inayoishi pamoja katika upendo, ushirikiano na mafundisho ya Kikristo kupitia Kanisa Katoliki inayotawaliwa na Neema ya Mungu na kuwajibika katika Kristo wa ubatizo wetu.